1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Kura zaendelea kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais Chad

7 Mei 2024

Kura zinahesabiwa nchini Chad baada ya kufanyika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kuhitimisha miaka mitatu ya utawala wa kijeshi kwenye taifa hilo la Afrika ya Kati.

https://p.dw.com/p/4fZBK
Chad N'Djamena 2024 | Uchaguzi
Karatasi ya kupigia kura uchaguzi wa Mei, 2024 nchini Chad.Picha: Desire Danga Essigue/REUTERS

Baadhi ya vituo vya kupigia kura kwenye mji mkuu N`Djamena vilibakia wazi hadi machweo lakini zoezi la kuhesabu kura lilikuwa limeanza karibu kote nchini humo usiku wa kuamkia leo.

Kiongozi wa sasa wa kijeshi Mahamat Idris Deby Itno anawania kuchaguliwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo baada ya kuitawala Chad kwa miaka mitatu tangu Aprili 2021. Aliingia madarakani kufuatia mauaji ya baba yake Idris Deby aliyekuwa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo.

Mahamat anatarajiwa kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo ambao wapinzani wake wamesema ni wa ulaghai. Mpinzani wake mkuu ni mwanasiasa aliyepitia misukosuko Succes Masra ambaye ameahidi mageuzi makubwa iwapo atashinda. Matokeo matokeo kamili yatatolewa ifikapo Juni 5.