1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaonya kuhusu uwezekano wa mashoga kushambuliwa

18 Mei 2024

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imewaonya raia wake walio ugenini kuhusu uwezekano wa mashoga na matukio ya jamii hiyo kushambuliwa na watu wanaochochewa na makundi ya kigaidi.

https://p.dw.com/p/4g1NM
Jamii ya LGBTQ wakiwa kwenye sherehe zao
Jamii ya LGBTQ wakiwa kwenye sherehe zaoPicha: Carlos Garcia Granthon/ZUMA Press Wire/picture alliance

Taarifa hii inawataka Wamarekani kuchukua tahadhari wanaposafiri bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi au kutaja vitisho vinavyoongezeka dhidi ya jamii ya LGBTQ. Hivi karibuni, baadhi ya nchi zimepitisha sheria kali  dhidi ya mashoga.

Soma pia: Biden akosoa sheria ya Uganda dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuhimiza kufutwa

Mwezi uliopita, Bunge la Iraq liliidhinisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa mashoga na watu waliobadili jinsia huku Mahakama ya Uganda nayo ikipitisha sheria inayotoa hukumu ya kifo kwa vitendo vinavyotajwa kuwa "ushoga uliokithiri."