1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Visa vya kipindupindu vyaripotiwa Kenya kufuatia mafuriko

8 Mei 2024

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake baada ya visa vya ugonjwa wa Kipindupindu kuripotiwa nchini Kenya ambayo imekumbwa na mvua kubwa na mafuriko katika wiki za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4fcSJ
Mafuriko Kenya
Wagonjwa wa Kipindupindu wameripotiwa katika Kaunti ya Tana River, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko.Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema wagonjwa 44 wa Kipindupindu wameripotiwa katika Kaunti ya Tana River, moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko.

Soma pia: Ruto aahidi kuhamishwa wananchi ambao wamekubwa na mafuriko

Mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya, Stephen Jackson, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Citizen, alisema anaamini kuwa kwa ushirikiano kati ya serikali na washirika wa kitaifa na kimataifa, watafanikiwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizochapishwa na vyombo vya habari vya ndani, mafuriko nchini Kenya yamesababisha vifo vya watu 238 huku zaidi ya watu wengine 200,000 wakiwachwa bila makao rasmi.