1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wauawa katika shambulizi mashariki ya Kongo

Mitima Delachance8 Mei 2024

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watu saba wameuawa na wengine sita kujeruhiwa vibaya usiku wa kuamkia Jumatano kufuatia mashambulizi ya mabomu katika kijiji kimoja kinachopakana na jimbo la Kivu Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4fdNe
Mji wa Minova karibu na ziwa Kivu
Mashambulizi ya waasi wa M23 yalisababisha vikosi vya Kongo na wakaazi kukimbilia mji wa MinovaPicha: ALEXIS HUGUET/AFP

Jospin Magambo ni katibu wa ofisi ya mamlaka ya serikali katika eneo la Minova wilayahi Kalehe. Anathibitisha kutokea kwa tukio hili na anakumbusha matukio mengine ya mashambulizi ya mabomu huko Minova, hali ambayo inaongeza wasiwasi kwa raia:

Soma pia: Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya Goma

Msemaji wa jeshi la Kongo katika jimbo la Kivu Kusini, Luteni Dieudonné Kajibwami, alikataa kuithibitishia DW kutokea kwa mashambulizi hayo, lakini alisema anafuatilia tukio hili ili kutambuwa kwa kina yaliyojiri.

Tukio hili lilijiri muda mfupi baada ya wengine watu 18 kuuawa katika mashambulizi ya hivi majuzi katika kambi nne za watu waliokimbia makaazi yao mashariki mwa mji wa Goma, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema jana Jumanne.

Waasi wa M23 katika eneo la Kibumba
Waasi wa M23 wanaendelea kuendesha harakati zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Baadhi ya asasi za kiraia wilayani Kalehe inawalaumu vijana yenye silaha wanaojiita Wazalendo, ambao huzozana kila mara hadi kufikia kufyatuliana risasi katika baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo.

Soma pia: 

Jumapili mchana, makundi manne yenye silaha yalipambana katika kijiji cha Bunyakiri ambako Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, Monusco, kilijiondoa wiki tatu zilizopita. Mapambano hayo yalisababisha kifo cha mpiganaji mmoja.

Asasi za kiraia zinaelezea kutokea matukio mengi kama hayo na zinayahusisha na kuripuka mara kwa mara kwa mabomu katika mipaka kati ya Wilaya ya Kalehe/Kivu Kusini na Wilaya ya Masisi/Kivu Kaskazini, hasa maeneo ya Ufamandu na Mupfunyi-shanga.

Tshisekedi: Amani imo mikononi mwa rais atakayemrithi Kagame

Eneo kulikotokea mapambano hayo yote ni mbali na kijiji ambacho watu saba waliuawa kwa mabomu.

Delphin Birimbi ni Msimamizi wa Mfumo wa mashauriano ya asasi za kiraia ndani ya wilaya ya Kalehe, anaiomba Serikali ichukue majukumu yake ya kuilinda ardhi ya Kongo kwa mujibu wa katiba ya nchi na kutafuta suluhisho la kudumu kwa suala la makundi yenye silaha yanayojiita Wazalendo kwa vile baadhi wanatatiza usalama wa raia:

Asasi za kiraia wilayani Kalehe zinaonya pia juu ya hali ya kibinaadamu inayozidi kuwa ngumu kwa wakimbizi waliotoka eneo la Masisi waliokimbia mapigano kati ya M23 na jeshi la Kongo, FARDC, na ambao bado wanakabiliwa na miripuko ya mabomu katika eneo walilokimbilia.